Wahandisi Washauri nchini watakiwa kusimamia kwa karibu ujenzi wa miundombinu ya barabara

TABORA-Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Miundombinu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mhandisi Rogatus Mativila amewataka Wahandisi Washauri wanaosimamia miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara nchini kusimamia kwa ukaribu miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati.Mhandisi Mativila ameyasema hayo leo Juni 10,2024 wakati akikagua ujenzi wa jengo la ofisi la wahandisi katika manispaa ya Tabora ambalo lipo chini ya mradi wa TACTIC inayosimamiwa na TARURA.
“Mhe. Rais anahangaika kutafuta fedha ili kuhakikisha wananchi wanapata barabara,wataalamu lazima mbadilike na kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa miradi hii huyu angekuwa anasimamiwa kwa ukaribu angeshakuwa amemaliza hapa.”

Hata hivyo, Mhandisi Mativila amewataka wataalam hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa ujenzi ili wakandarasi wakamilishe kazi kwa wakati.

Aidha, amemtaka Mhandisi Mshauri UNITEC Civil Consultants Ltd kuhakikisha anasimamia kwa karibu ujenzi huo na ifikapo mwezi Agusti mwaka huu jengo hilo liwe limekamilika

Ujenzi wa jengo la ofisi la wahandisi linalogharimu takriban milioni 800 lilianza ujenzi wake Novemba 2023 na lilitarajiwa kukamilika 15 Juni,2023 na kuagiza ujenzi huo uwe umekamilika ifikapo Agosti 2024 na linajengwa na mkandarasi CICO Contractor.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news