Wahukumiwa kwa kuwahonga Polisi ili wasiwakamate

RUVUMA-Wakulima wawili wamehukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini shilingi milioni moja kwa kutoa hongo shilingi 600,000 kwa maofisa wa Polisi Ofisi ya OC-CID Songea.
Ni baada ya leo Juni 24, 2024 kuamuliwa kesi ya Jinai Na.17134/2024 mbele ya Mheshimiwa Lilian Ernest Rugarabamu (PRM) Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi katika Mahakama ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Katika shauri hilo lililoendeshwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi,Mwinyi Yahaya, mshtakiwa wa kwanza Bw. Emmanuel Ambrose Komba na Mshitakiwa wa pili Bw. Festo Dominicus Komba wote wakulima walishtakiwa kwa kosa la kutoa hongo hiyo.

Ikiwa ni kinyume na kifungu cha 15 (1) (b) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Sura ya 329, Mapitio ya Mwaka 2022) kwa A/INSP Wazo Michael Mwang'onda na G.1868 D/CPL Patrick kutoka Ofisi ya OC-CID Wilaya ya Songea.

Lengo ni ili wasiwakamate kwa kosa la kulima bangi na kukutwa na bangi kwenye shamba katika Kijiji cha Ngongosi kufuatia msako ulioendeshwa na polisi hao.

Mahakama imewahukumu kulipa faini ya shilingi 500,000 kwa kila mshtakiwa au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Pia,Jamhuri imeomba kutaifisha fedha shilingi 600,000 zilizotolewa na washitakiwa kwa ajili ya kuwahonga polisi na kuwa fedha za Serikali.

Aidha,Mahakama imeridhia ombi la Jamhuri na kutaifisha fedha hizo na kuelekeza Jamhuri kuziweka akaunti ya DG PCCB Hazina. Washtakiwa wamelipa faini jumla ya shilingi 1,000,000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news