Wakamatwa Longido wakitorosha ng'ombe 70

ARUSHA-Jeshi la Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne na mifugo 70 aina ya ng’ombe ambayo ilikuwa ikitoroshwa Kwenda nchi Jirani kinyume na utaratibu huku likitoa onyo kwa watu wanaojihusisha na tabia hiyo.
Kamanda wa kikosi hicho,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Simon Pasua ameyasema hayo leo Juni 10,2024 wilayani Longido Mkoa wa Arusha.

Amesema, kikosi hicho kinaendelea na operesheni yake nchi nzima ya kuwabaini baadhi ya watu wanaotorosha mifugo na kukwepa taratibu zilizopo.
SACP Pasua amesema, watuhumiwa hao waliokamatwa wakisafirisha mifugo hiyo 70 majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi huku akiweka wazi kuwa kikosi hicho tayari kina majina ya watu wanaojihusisha na utoroshaji wa mifugo ambapo amesema, watuhumiwa hao pia watakamatwa wakati wowote.

Kamanda Pasua amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu wanaojihusisha na utoroshaji wa mifugo ili jeshi hilo liwachukulie hatua za kisheria wahusika wa vitendo hivyo.
Nao baadhi wananchi wa Wilaya ya Longido Kata ya Namanga Mkoa wa Arusha wamesema kuwa,watu ambao watabainika kuhusika katika matukio hayo wanapaswa kukamatwa na vyombo vyao vya usafiri wanavyotumia kutaifishwa ili matukio kama hayo yaweze kupungua hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news