Walimu Kakonko badilikeni hali ya elimu ni mbaya-Dkt.Msonde

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde amewataka walimu wa shule za msingi na sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kubadilika kiutendaji, kwani hali halisi ya elimu katika halmashauri hiyo ni mbaya kutokana ufanyaji kazi wa mazoea.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Dkt. Charles Msonde akizungumza na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na maafisa hao.

Dkt. Msonde ametoa wito huo kwa walimu wa halmashauri hiyo ya Kakonko, wakati wa kikao kazi chake na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu, kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Kakonko.

“Hali halisi ya Kakonko kwenye elimu ni mbaya, wapo wanafunzi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu na kuongea kuwa Kakonko haijafikia malengo ya kitaifa na kuwa na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu kwa zaidi ya asilimia 50,” Dkt. Msonde amefafanua.Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi chao na Naibu Katibu Mkuu huyo.

Dkt. Msonde amesema, ufaulu wa shule ya msingi si mzuri ndio maana watoto wengi wa Kakonko hawapati ufaulu utakawawezesha kujiunga na elimu ya sekondari, hivyo taarifa iliyowasilishwa na Afisa Elimu ikianisha kuwa Kakonko ina ziada ya madarasa ya sekondari si kweli kwani ziada hiyo inatokana watoto kukosa sifa ya kujiunga na sekondari.

Dkt. Msonde amehimiza kuwa, walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko wanapaswa kuacha utamaduni wa kufanya kazi kwa mazoea ili kuongeza kiwango cha ufaulu.

“Walimu mkiendelea kuruhusu mtoto avuke elimu ya awali na darasa la kwanza bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu ni kosa na mnamuua kiakili kwani mkitaka msingi wa elimu kwa mtoto uwe bora mnapaswa kuhakikisha anajua kusoma, kuandika na kuhesebu,” Dkt. Msonde amesisitiza.Katibu Tawala wa Wilaya ya Kakonko Bw. Maulid Mtulia akitoa neno la shukrani kwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde (hayupo pichani) mara baada ya Naibu Katibu Mkuu huyo kufanya kikao kazi na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kakonko Bw. Maulid Mtulia amemhaidi Dkt. Msonde kuwa, watajipanga kuhakikisha watoto wote wa darasa la awali na la kwanza wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu ikiwa ni pamoja na kuwapanga walimu mahiri katika darasa la tatu ili watengeneze msingi bora wa elimu kwa watoto.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu),Dkt. Charles Msonde akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kikao kazi chake na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.

Dkt. Msonde amehitimisha siku ya kwanza ya ziara yake kuhimiza uwajibikaji mkoani Kigoma kwa kufanya vikao kazi na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na Walimu waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na Kibondo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news