Wanakijiji washauriwa kuweka akiba kwenye vikundi vilivyosajiliwa

NA EVA NGOWI
WF

SERIKALI imewataka wananchi kuweka akiba ya fedha zao kwa kuwa akiba ni sehemu mojawapo ya mapato ambayo mwananchi, mfanyabiashara au mjasiriamali anaweza kuhifadhi sehemu salama kwa ajili ya kutimiza malengo aliyojiwekea.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha- Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro, akitoa elimu ya fedha kwa Wanavikundi na Wajasiriamali wadogo wadogo katika Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.

Akitoa elimu kwa wananchi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini Afisa uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi, Bw. Omar Bakari, alisema ni muhimu kuwa na fedha ya dharura ambayo itasaidia wakati litakapotokea tukio lisilotarajiwa.
Afisa Msimamizi wa Fedha Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha- Wizara ya Fedha Bw. Jackson Mshumba, akitoa elimu ya fedha kwa Wanavikundi na Wajasiriamali wadogo wadogo katika Ukumbi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.

“Tunaposema tukio la dharura ni kama ajali, misiba, kupoteza kazi, msimu wa njaa na mazingira mengine ambayo hayakutarajiwa,"amesema Bw. Bakari.

Bw. Bakari alisema akiba inaweza kuhifadhiwa Benki, Vikundi au SACCOS zilizosajiliwa kwa mujibu wa sheria.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha- Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro (kushoto) akimkabidhi Mjasiriamali Bi. Magreth Kainuka, fulana wakati wa utoaji elimu ya fedha katika Ukumbi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.
Wanavikundi na Wajasiriamali wadogo wadogo wakifuatilia filamu ya Elimu ya Fedha iliyokuwa ikioneshwa katika Ukumbi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.
Wanavikundi na Wajasiriamali wadogo wadogo wakifuatilia filamu ya Elimu ya Fedha iliyokuwa ikioneshwa katika Ukumbi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.
Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Bw. Winfred Mwamkalaba (kushoto), akimkabidhi mwanakikundi mjasiriamali Bw. Ruben Masinga, fulana wakati wa utoaji elimu ya Fedha katika Ukumbi wa Kijiji cha Muze Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.

Aidha, Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Bw. Winfred Mwamkalaba, alisema kuwa baadhi ya wakazi wa Sumbawanga walizoea kufanya mambo kwa mazoea lakini baada ya huo mfumo wa Huduma Ndogo za Fedha kuanzishwa na kutoa elimu na kuwepo kwa waratibu walioko kwenye halmashauri zingine za mkoa wa Rukwa, imeamsha ari na wengi wanajitokeza kusajili vikundi vyao.
Timu ya wataalamu wanaotoa elimu ya fedha Mkoa wa Rukwa kutoka kushoto Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha- Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro, Afisa uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi, Bw. Omar Bakari na Afisa Msimamizi wa Fedha Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha- Wizara ya Fedha Bw. Jackson Mshumba.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Wizara ya Fedha).

“Nitoe wito kwa wananchi wengine ambao wanafanya shughuli zao bila kusajiliwa wafike Ofisi za Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga au wataalamu kutoka kwenye kata ambao wanafanya kazi hizo kwa ajili ya kuwapa miongozo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusajili vikundi vyao."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news