Wastaafu kuweni makini dhidi ya matapeli-Wizara ya Fedha

NA EVA NGOWI

SERIKALI imewaasa wastaafu na wastaafu watarajiwa kuwa makini na matapeli, kuanzisha biashara wasizokuwa na uzoefu nazo pamoja na kuepuka washauri wasiokuwa na nia nzuri ambao wanataka kujinufaisha wao wenyewe.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Salim Kimaro akitoa elimu ya kujipanga kuhusu maisha ya kustaafu iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa.

Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Salim Kimaro aliyasema hayo alipokuwa akitoa semina ya Elimu ya Fedha kwa wanavikundi na wajasiriamali wadogo katika ukumbi wa Ofisi za Halmashauri Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa.

Bw. Kimaro alisema kumekuwa na wimbi la matapeli wanaotoa ushauri usiofaa kwa wastaafu na pia kwa wale walioko kwenye mifuko ya kijamii wamekuwa wakitapeliwa kwa kupigiwa simu huku wakiomba fedha na kuwaahidi kuwa watawasaidia walipwe mafao yao haraka.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Salim Kimaro (kulia) akisalimiana na kumkabidhi Kaimu Mkurugenzi na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Bw. Wambura Sunday (kushoto) “flash” yenye filamu ya elimu ya fedha kwa ajili ya kuwaonesha wananchi wa Halmashauri hiyo ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria semina hiyo.

“Kumekuwa na wimbi la matapeli wanatoa ushauri usiofaa kwa wastaafu kwa kuwa wanafahamu sasa wamepata hela nyingi za kiinua mgongo, kwa hiyo kila mmoja anakwenda kumshauri lakini ushauri ule unakuwa kwa ajili ya kuwanufaisha wao wenyewe.
Kaimu Mkurugenzi na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, mkoani Rukwa, Bw. Wambura Sunday akiwasikiliza wataalamu wa utoaji elimu ya fedha (hawamo pichani) mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo.

"Hivyo tunatoa rai wastaafu wawe makini sana na ushauri wanaopewa na hawa watu ili wasiingie kwenye hii kadhia ya kutapeliwa na endapo itatokea ukapigiwa simu ya kudai chochote ili upate mafao yako kwa wakati au kwa haraka tafadhali toa taarifa kwa Mfuko wowote wa Hfadhi ya Jamii uliopo ili suala hilo lifuatiliwe na kuchukuliwa sheria,”amesema Bw. Kimaro.
Baadhi ya wanavikundi, wastaafu, wajasiriamali pamoja na watoa elimu ya fedha wakifuatilia filamu ya elimu ya fedha iliyokuwa ikioneshwa katika Ofisi za Halmashauri Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa.

Aidha, Bw.Kimaro, aliwashauri wastaafu na wastaafu watarajiwa kuwa wanapaswa kujiandaa kustaafu pindi wanapopata ajira au siku ya kuanza kupata kipato kwa kuwa na tabia ya kujiwekea akiba kwenye taasisi, vikundi au SACCOS zilizosajiliwa kwa ajili ya maisha ya baadae.
Timu ya Wataalamu ya Utoaji Elimu ya Fedha pamoja na baadhi ya maafisa kutoka Mkoa wa Rukwa katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Afisa Usimamizi wa Fedha- Wizara ya Fedha, Bw. Jackson Mshumba, Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bw. Omar Bakari, Kaimu Mkurugenzi na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Bw. Wambura Marwa, Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha Wilaya ya Kalambo, Bw. Iddy Seleman Mohamed na Afisa Biashara Manispaa ya Sumbawanga, Bw. Amani Marsel.

Serikali inaendelea kutoa elimu kwa umma, ikiwa na lengo la kuwafikia Watanzania wote na kuwajengea uwezo wa uelewa kuhusu masuala ya fedha, kuweka akiba, uwekezaji, usimamizi wa fedha binafsi, kujipanga kuhusu Maisha ya kustaafu pamoja na masuala ya usimamizi wa sheria na kanuni za huduma ndogo za fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news