Wataalamu NIRC wanolewa usalama wa mabwawa kuinusuru reli ya kati

DODOMA-Wataalamu wa Tume ya Taifa ya Uwagiliaji (NIRC) washiriki mafunzo juu ya usalama wa mabwawa na matayarisho ya ujenzi wa mabwawa ikiwa ni miongoni mwa hatua za awali katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi na ukarabati wa mabwawa sita ya umwagiliaji ya kuvuna maji,kuzuia mafuriko na kulinda reli ya kati katika mikoa ya Dodoma na Morogoro.
Mafunzo hayo yametolewa jijini Dodoma na wataalamu kutoka Benki ya Dunia kwa lengo la kuwakumbusha wataalamu kuzingatia usalama wa mabwawa katika hatua za awali za utekelezaji ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea ikiwemo vifo pamoja na uharibifu wa makazi na miundombinu mingine.
Katika mafunzo hayo wataalamu wamepatiwa elimu ya kutambua viashiria vya vihatarishi vya mabwawa pamoja na namna bora ya kujiandaa ili kupunguza au kukabili madhara yanayoweza kutokea ikiwa mabwawa yatakoyojengwa na yanayoendelea kujengwa, yataonesha dalili zozote za hatari.
Vilevile wataalamu wamekumbushwa kuhusu sera na sheria za mabwawa na wataalamu kutoka Wizara ya Maji, ambapo lengo la mafunzo hayo pamoja na kujenga uwezo wa usalama wa mabwawa pia itasaidia miundombinu hiyo kudumu kwa muda mrefu zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news