Watumishi wa umma waonywa ukopaji kwa wakopeshaji wasio rasmi

NA CHEDAWIE MSUYA
WF

WATUMISHI wa umma wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wametakiwa kuacha tabia ya kujihuisha na ukopaji wa fedha katika taasisi zisizo rasmi ambazo mara nyingi huwa na riba kubwa na kusababisha migogoro wanaposhindwa kulipa kwa wakati.
Matukio ya picha yakionesha wananchi wakifuatilia semina inayotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi wa Kigoma kupitia filamu inayofikisha ujumbe kwa njia ya kuvutia na inayoeleweka na kuweza kuwa zana nzuri ya kufikisha ujumbe kwa wananchi wa Kigoma na kuwapa elimu muhimu kuhusu fedha na uwekezaji ili kusaidia kubadilisha mwelekeo wao kuelekea maisha bora na ustawi wa kifedha.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).

Akizungumza na timu ya wataalamu wa fedha kutoka wizara ya fedha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Dkt. Gabriel Chitupila, alisema kuwa mivutano baina ya watumishi na wakopeshaji wasio rasmi huathiri utendaji katika sehemu za kazi na kuhatarisha utumishi wa mkopaji.
Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akitoa semina kwa wananchi wa kata ya Kibondo mkoani Kigoma, kuhusu umuhimu wa elimu ya fedha na njia bora za kujikwamua kiuchumi na kibiashara.

Dkt. Chitupila alisema kuwa hali hiyo husababisha kushusha ari ya watumishi kufanyakazi kutokana na muda mwingi wakijikuta wanakimbizana na wakopeshaji hasa pale mkopo unapokuwa mkubwa na kushindwa kulipa hivyo akawasihi kama kuna ulazima wa kukopa wazitumie taasisi ambazo zimesajiliwa ili wapate huduma yenye uhakika isiyo kandamizi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma, Dkt. Gabriel Chitupila, akizungumza na Timu ya watalaamu kutoka Wizara Fedha, Ofisini kwake, kuhusu umuhimu kwa watumishi kufanya kazi na taasisi au mashirika ya kifedha yaliyo rasmi na yanayofuata taratibu za kisheria za mikopo ili kupunguza mivutano na kuleta utulivu katika maeneo ya kazi, huku ikilinda utumishi wa watumishi.

“Tatizo la mikopo “kausha damu” lipo na linawakumba hadi watumishi wa umma hasa walimu, unakuta mwalimu hakai ofisini akiogopa kutafutwa na wakopeshaji au kulazimika kutoroka katika kituo chake cha kazi kwenda kufanya vibarua sehemu nyingine ili pate hela za kulipa deni na kusababisha wanafunzi kukosa haki yao ya msingi ya kufundishwa, nitoe rai wenye tabia hiyo waache mara moja” alıonya Dkt. Chitupila.
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma, Kanali Agrey Magwaza, akizungumza na Timu ya watalaamu kutoka Wizara Fedha, Ofisini kwake, kuhusu umuhimu kwa watumishi kufanya kazi na taasisi au mashirika ya kifedha yaliyo rasmi na yanayofuata taratibu za kisheria za mikopo ili kupunguza mivutano na kuleta utulivu katika maeneo ya kazi, huku ikilinda utumishi wa watumishi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Kanali Agrey Magwaza, aliwahimiza Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Huduma Ndogo za Fedha ngazi ya Halmashauri kufuatilia na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kifedha ili kuwasaidia kuwa na uelewa juu ya masuala mbalimbali ya huduma hizo.

"Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Huduma za Kifedha katika halmashauri tufahamu kuwa kipimo chetu sisi watumishi wa umma ni namna tunavyo wahudumia wananchi na kuona wanavyoridhika na huduma kwa kulimaliza tatizo la kuwepo kwa watoa huduma wanaoweka riba kubwa na kukiuka sheria za nchi, hicho ndicho kitakuwa kipimo chetu cha utumishi,"alisema Kanali Magwaza.

Aidha, Magwaza alisema kuwa ni rahisi sana mtu kukopo wakati anaona riba ni kubwa lakini akianza kukatwa fedha ndio anaona fedha ni kubwa na mwishowe anajuta.
Afisa Biashara RS Kigoma, Bw. Baraka Mphubusa, akitoa mada kwa wananchi wa Kibondo kuhusiana na umuhimu wa elimu ya fedha inayolenga kuwawezesha wananchi kupata maarifa na mbinu za kifedha.

"Mtu anaona riba ni kubwa lakini anaona sawa tu na anapoanza kukatwa fedha zake ndipo anakunywa ba msongo wa mawazo na hatimaye mtu huyo anapoteza mwelekeo,"alisisitiza Kanali Magwaza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news