Waziri Mhagama aipongeza Sukos Kova Foundation kwa kuandaa mafunzo ya uokoaji

DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amepongeza taasisi ya Sukos Kova Foundation na taasisi ya Peaceland Foundation kwa pamoja kwa kushirikiana taasisi za uokoaji Serikalini kwa kuandaa mafunzo maalumu ya uokoaji kwenye maji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akipokea jaketi la uokoaji (Life Jacket) Kutoka kwa Kamishina Mstaafu Selemani Komba lilotolewa Maalumu kwa ajili ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya kufungua mafunzo hayo yaliyohusisha vikosi vya Jeshi la Polisi Wanamaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na vikundi mbalimbali vya uokoaji katika ngazi ya jamii iliyofanyika Juni 9, 2024 Sawasawa Bay Mikocheni, Dar es salaam.

Amesema,boti iliyokabidhiwa Ofisi ya Waziri Mkuu itaenda kwenye maziwa mito na maeneo mbalimbali ili ikakutane na taasisi za uokoaji na vikundi vya jamii ambavyo vitakuwa tayari kwa mafunzo.
"Maamuzi hayo ni ya kizalendo na tutaendelea kuheshimu uwepo wa taasisi hizo binafsi, ikiwa ni pamoja na utaratibu ambao zitakuwa zimejiwekea katika kuleta tija kubwa kwa taifa na ustawi wa Watanzania.”

Aliongezea kuwa,matumizi ya uokoaji yanaenda sambamba na matumizi ya vifaa hivyo na kutoa wito juu ya utoaji wa elimu kuhusu matumizi sahihi ya vifaa, kwa wakati sahihi na mahali sahihi pale ambapo vitahitajika ili viweze kukabiliana na maafa pindi yanapotokea.

"Boti iliyokabidhiwa ni boti ya kisasa na kwa sababu mambo ya uokoaji ni mambo mtambuka yataenda sambamba na uzuiaji wa uhalifu, na inaweza kutumika pia kuzuia uhalifu kwenye maeneo ya maji katika Taifa letu,”alisema Mhe.Mhagama.

Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kushirikiana na taasisi nyingine za kiraia ili kuweza kufika maeneo mbalimbali yenye uhitaji wa kupata mafunzo ya uokoaji.
Aidha,alitoa rai kwa taasisi za uokoaji na vikundi vya uokoaji kuhakikisha wanatunza vifaa vilivyotolewa ili viweze kudumu kwa muda mrefu huku vikiendelea kutoa msaada wa uokoaji.

"Watakaopokea mafunzo watumie vizuri maarifa hayo ili waweze kufunza wengine na kusaidia kundi kubwa kunufaika na mafunzo hayo ambayo yatatolewa kwa muda wa wiki mbili.

"Ni vyema taasisi za uokoaji na vikundi vya uokoaji vikatumia elimu itakayotolewa kwa uzalendo mkubwa pindi tutakapokutana na majanga ya maafa.”

Waziri Mhagama alizikumbusha taasisi Sukos Kova Foundation kuendelea kufungua milango ili taasisi nyingine ambazo zinapenda kufanya ushirikiano na taasisi hiyo kwenye masuala ya uokoaji wawe tayari kushirikiana.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt, Koba Nguvila amesema Mkoa wa Dar es salaam unaguswa kwenye habari ya uokoaji na mafaa kwa sababu Mkoa huo unapata mafuriko na madhila ya kuchafuka kwa bahari.
Amesema kuwa, hili ni jambo la faraja kwa taifa, pindi inapotokea jamii imezungukwa na maji unatumia vifaa vya kisasa vya uokoaji hivyo kusaidia kuimarisha usalama wa kuokoa watu.

Naye Kamishna Mstaafu Suleiman Kova, amesema,Sukos Kova Foundation kwa kushirikiana taasisi ya Peaceland Foundation wametoa boti moja ili liweze kuogeza nguvu katika miundombinu iliyopo kazini.

"Tumeona tumpatie Jaketi la Uokoaji (Life JacketRais) Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa sababu amekuwa mstari wa mbele kutoa maelekezo makubwa wakati maafa yanapotokea,"alisema.

Awali Mkuu wa Wajumbe kutoka Peaceland Foundation,Bi. Jing Ping, amesema nchi ya China na Tanzania wamekuwa na ushirikiano na mshikamano wa karibu kwa zaidi ya miongo sita sasa.

"Nchi zetu zimekuwa zikisaidiana katika mambo mbalimbali na tukio la leo ni moja ya ushahidi wa ushirikiano wetu, na katika hili taasisi yangu kwa kushirikiana na Sukos Kova Foundation zimejikita katika kuimarisha juhudi za kukabiliana maafa kwa kutoa vifaa mbalimbali vya kusaidia uokoaji."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news