DAR-Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameongoza Kikao cha 11 cha Kamati ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongoza Kikao cha Kumi na Moja cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika tarehe 09 Juni, 2024 Ukumbi wa Mikutano wa JNCC Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa wakati wa Kikao cha Kumi na Moja cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika tarehe 09 Juni, 2024 Ukumbi wa Mikutano wa JNCC Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, Salum Kassim Ali na kulia ni Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Balozi Mohamed Haji Hamza.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Adolf Mkenda akizungumza na baadhi wa Kikao cha Kumi na Moja cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi 2022, Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu.