DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 22, 2024 atazindua ripoti ya Kidemografia, Kijamii, Kiuchumi na Mazingira zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi na Sensa ya Majengo ya Mwaka 2022.
Katika uzinduzi huo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi Hemed Seleman Abdulah pia atashiriki.