Wizara ya Elimu yapokea maelekezo ya Katibu Mkuu wa CCM kuhusu boom vyuoni

KILIMANJARO-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema, wizara yake imepokea maelekezo ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi kuhusu suala la ‘boom’ kwa wanafunzi wa vyuo nchini.

Dkt Nchimbi akiwa eneo la Usa River jana Juni 4,2024 Wilaya ya Arumeru alitoa maagizo kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha wanafunzi wa vyuo wanalipwa fedha hizo ifikapo mwisho wa mwezi Juni.
Profesa Mkenda ambaye ni Mbunge wa Rombo akizungumza kwenye kikao cha ndani cha viongozi na mabalozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoani Kilimanjaro mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, amesema kuwa, wizara yake imepokea agizo hilo na kwamba watalitekeleza kabla ya mwisho wa mwezi.

“Ndugu Katibu Mkuu jana pale Arusha ulitoa maelekezo kuhusu suala la boom na naomba nitumie nafasi hii kusema kuwa suala hilo tutalifanyia kazi na kabla ya muda uliyotoa wanafunzi wote nchini watalipwa,”alisema.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Komredi Amos Gabriel Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Hamid Abdalla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news