Wizara ya Fedha yakamilisha tafiti mbili maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Fedha, Mheshimiwa Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba amesema, hadi Aprili 2024, wizara imefanikiwa kukamilisha tafiti mbili kwenye maeneo ya maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi sawa na asilimia 50 ya lengo la mwaka.
Ameyasema hayo leo Juni 4, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2024/2025.

"Kwa mwaka 2023/24, wizara ilipanga kufanya tafiti nne kwenye maeneo ya maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi jumla ili kuwezesha maamuzi ya kisera.

"Aidha, wizara ilitarajia kufanya tathmini ya huduma za wizara kwa wadau na mapitio ya utekelezaji wa Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2023/24. 

"Hadi Aprili 2024, wizara imefanikiwa kukamilisha tafiti mbili sawa na asilimia 50 ya lengo la mwaka."

Vile vile, Mheshimiwa Waziri amesema,wizara imekamilisha tathmini ya huduma za wizara kwa wadau, mapitio ya utekelezaji wa Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2023/24.

Sambamba na kuandaa ikiwemo kusambaza Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2024/25.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news