Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb), akimkabidhi cheti maalumu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, kwa kuwa miongoni mwa wizara 10 zilizofanya kazi iliyotukuka ya kuhabarisha umma kuhusu, sera, programu, mipango, mikakati na matukio katika Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, Tukio alilolifanya kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, wakati akifunga Rasmi Kikao kazi cha 19 cha Maafisa Habari wa Serikali, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.