Wizara ya Madini yaahidi ushirikiano zaidi kwa wadau

LONDON-Wizara ya Madini imesema, itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha sekta hiyo inawaneemesha Watanzania na kupaisha uchumi wa Tanzania.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini,Kheri Mahimbali kupitia ujumbe alioutoa katika ukurasa wake wa Twitter (X) akiwa jijini London, Uingereza.
"Madini ni maisha na utajiri kwetu. Wiki hii nilipata fursa ya kukutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Helium One Bi. Lorna Blaisse nikiwa hapa jijini London, Uingereza.

"Pamoja na timu yangu, tumepata taarifa ya kazi nzuri inayoendelea kufanywa na kampuni hii katika kuikuza sekta ndogo ya gesi ya Helium. Tumewapongeza na kuwahakikishia kuendelea kuwaunga mkono katika majukumu yao.
"Kipekee tunapenda kuupongeza Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuvutia uwekezaji nchini, hususan kwenye sekta ya madini.

"Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki amekuwa kiongozi wa mfano na wa kuigwa katika kuunganisha sekta binafsi na serikali.
"Kuna masuala mengi yenye tija tunayoshirikiana na ofisi yake, kama vile kuwajengea uwezo watumishi wa sekta ya madini katika masuala ya Jiolojia, Jiomolojia na uchanganuzi mkubwa wa taarifa (big data analysis).

"Kuangalia namna ya kuvutia mitaji zaidi nchini kwenye sekta ya madini, pamoja na ushiriki wetu kwenye majukwaa ya kimataifa kama vile ya Chatham House na Financial Times Mining Summit."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news