📌Yaeleza juhudi za Serikali katika uendelezaji wa Nishati Jadidfu nchini
📌Mkakati na Mpango Kazi wa Kitaifa wa Nishati Jadidifu mbioni kuzinduliwa
DAR-Wizara ya Nishati imeshiriki Kongamano la Kitaifa la Nishati Jadidifu kwa mafanikio ambapo imetumia kongamano hilo kueleza juhudi zinazofanywa na Serikali katika uendelezaji wa Nishati Jadidifu nchini na hii ikijumuisha utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia.

Amesema, uzinduzi wa mkakati huo utaakisi vyema Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2015 na makubaliano mengine ya kimataifa na kitaifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.
"Kwa kuhama kutoka kwenye matumizi ya mimea asilia kama vile kuni na mkaa wa kupikia, hatupunguzi hewa chafu tu bali pia tunaboresha hali ya hewa na kuboresha maisha ya mamilioni ya watu, utekelezaji wa mkakati huu unasaidia moja kwa moja suala la nishati safi ya kupikia,"amesema Mha.Luoga.

Mha. Inocent Luoga aliwashukuru wafadhili mbalimbali waliowezesha Wiki hiyo kufanyika ikiwemo kampuni ya Sunking, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP); TANESCO, Ensol Tanzania Limited, Global Off- Grid Lighting Association (GOGLA); Africa Enterprise Challenge Fund (AECF) na Umoja wa Ulaya (EU).

Kaulimbiu ya Kongamano hilo ni "Nishati Mbadala kwa Uchumi Shirikishi na Kijani,'