World Vision kuendelea kusaidia jamii

NA RESPICE SWETU

SHIRIKA la World Vision Buhoma linalojihusisha na utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika tarafa ya Makere wilayani Kasulu, litaendelea kutoa huduma katika eneo hilo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Mradi wa World Vision Buhoma, Emmanuel Ntachombonye alipokuwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Makere wilayani Kasulu.

Amesema,Shirika la World Vision lililoratibu kufanyika kwa maadhimisho hayo, litaendelea kutoa huduma mbalimbali za kijamii kama ambavyo limekuwa likifanya katika muda wote.

Sanjari na kufanikisha maadhimisho hayo, idara za afya, elimu na maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu zimekuwa zikipata manufaa makubwa kupitia shirika hilo.

Miongoni mwa manufaa hayo ni ujenzi wa miundombinu katika zahanati, vituo vya afaya, shule na utoaji wa elimu na mafunzo ya aina mbalimbali kwenye jamii.

Aidha,World Vision kupitia mradi wa Buhoma, wamekuwa wadau wakubwa wa maendelea ya ya taaluma na michezo kwenye shule za msingi na sekondari wilayani Kasulu.

Washiriki wa maadhimisho hayo, walishuhudia mgeni rasmi kaimu katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Paul John akikabidhi vifaa vya michezo vya wavulana na wasichana kwa shule tano za msingi na mbili za sekondari vilivyotolewa na shirika hilo.

Shule za msingi zilizokabidhiwa vifaa hivyo ni Makere, Muungano, Nyarugusu, Kitagata na Nyanyuka huku shule ya Nyamidaho na Kimwanya zikipokea kwa upande wa shule za sekondari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news