DAR-Mbobezi wa kukuza nyimbo za injili, msambazaji na muandaaji wa matamasha ya injili Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, Mheshimiwa Alex Msama jana Julai 20, 2024 jijini Dar es Salaam ametunukiwa Tuzo ya Heshima.


Mbali na haho, ikumbukwe kuwa, Alex Msama amekuwa na mchango mkubwa katika kuufanya muziki wa injili kuendelea kufahamika na kupendwa zaidi ndani na nje ya Tanzania.
Licha ya kufahamika waimbaji wengi wameweza kuitumia fursa hiyo kujipatia vipato na kuziendea ndoto zao, kwani licha ya Msama kuupromoti muziki huo amekuwa msambazaji wa kazi hizo za injili huku akiandaa matamasha ya Kimataifa hapa nchini kila mwaka.