Msanii aliyechoma picha ya Rais akamatwa jijini Mbeya

MBEYA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Shadrack Yusuph Chaula (24), mkazi wa Kijiji cha Ntokela katika Kata ya Ndato wilayani Rungwe mkoani humo, baada ya kuchoma moto picha inayomuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga amesema kuwa, Juni 30,2024 mtuhumiwa huyo ambaye ni msanii wa sanaa ya uchoraji alijirekodi video fupi akitamka maneno makali ya kumkashifu Rais Dkt. Samia huku akichoma picha inayomuonesha Rais na kuisambaza mitandaoni.

Mapema leo asubuhi Julai 2, 2024, Mkuu wa mkoa wa Mbeya, alitoa saa 24 kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo kuhakikisha mtuhumiwa huyo anakamatwa.

Amesema, kitendo alichokifanya si cha kimaadili wala kiungwana na kiko tofauti na utamaduni halisi wa wakazi wa mkoa huo.

Ikumbukwe kuwa, Rais wa Jamhuri la Muungano ndiye Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serikali, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Vile vile, Rais ndiye kiongozi wa Utawala wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news