Askari Polisi wanne wafukuzwa na kufutwa kazi jeshini

DODOMA-Jeshi la Polisi Tanzaniza limewafukuza kazi na kuwafuta Jeshini Trafiki wanne baada ya kuwashtaki kijeshi na kuwakuta na hatia.

Ni kufuatia uchunguzi uliobaini kuwa askari hao walikuwa wamefuta picha kutoka kwenye camera za Jeshi la Polisi walizokuwa wanatumia kupima mwendokasi wa madereva waliokuwa wamekiuka sheria za usalama barabarani kwa maslahi yao binafsi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Julai 9,2024 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David A. Misime.

“Mtakumbuka Mei 30,2024, Jeshi la Polisi lilitoa taarifa ya kushikiliwa Askari Polisi wanne kwa ajili ya uchunguzi, askari hao walikuwa wanafanya kazi kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro na baada ya uchunguzi kukamilika ilibainika kuwa, askari hao walikuwa wamefuta picha kutoka kwenye kamera za Jeshi la Polisi walizokuwa wanatumia kupima mwendo kasi wa madereva waliokuwa wamekiuka sheria za usalama barabarani, kwa maslahi yao binafsi.

“Walishtakiwa kijeshi na wakapatikana na hatia na Julai 8,2024 walifukuzwa kazi na kufutwa Jeshini;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news