ATCL yadhamiria kwenda Msumbiji,Balozi Kasike aahidi ushirikiano

DAR-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji,Mheshimiwa Phaustine Kasike amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi.
Mkutano wao umefanyika kwenye ofisi za shirika hilo zilizopo jijini Dar es Salaam ambapo viongozi hao wamejadiliana namna ambavyo ndege za Shirika la ATCL zitaanza safari zake za abiria na mizigo kati ya Tanzania na Msumbiji.
Katika mkutano huo, Mhe. Balozi Kasike ameahidi kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji utatoa kila aina ya ushirikiano ili kuhakikisha ATCL inaanza safari za Msumbiji kama ilivyopangwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news