Balozi Kasike,Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE wakubaliana

DAR-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Balozi Phaustine Kasike amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mkutano huo ulifanyika kwenye Ofisi za TANTRADE zilizopo kwenye Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam ambapo viongozi hao wawili walikubaliana kushirikiana katika kutafuta wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Msumbiji kwa ajili ya kuja kuwekeza na kufanya biashara nchini Tanzania. Wakati wa mkutano huo, TANTRADE iliahidi kushiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Jijini Maputo (FACIM) yatakayofanyika Msumbiji mwezi Agosti, 2024 sambamba na wadau wengine ili kutangaza fursa mbalimbali za kibiashara na Uwekezaji zilizopo Tanzania.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Kasike aliahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kwa TANTRADE ili kuwafikia Wafanyabiashara na wadau wengine muhimu waliopo Msumbiji ili kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news