Balozi Nchimbi asimamishwa Ndanda, ampigia simu Waziri wa TAMISEMI

MTWARA-Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo Julai 28,2024 akiwa njiani kuelekea Mtwara Mjini baada ya kuzungumza na Wananchi na Wanachama wa Masasi amesimamishwa na wananchi katika eneo la Kata ya Nganganga Jimbo la Ndanda wakitaka awasalimie na kuzungumza nao.
Akiwa hapo Katibu Mkuu Balozi Nchimbi ameendelea kuwasisitiza Watanzania kuhusu umuhimu wa umoja wa kitaifa kwa kutunza tunu ya amani iliyopo nchini, pamoja na kumpigia simu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa akitaka kujua utekelezaji wa ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Afya, ambapo Waziri alipokea maelekezo na kuahidi kuwa ujenzi utaanza mwezi ujao baada tu ya mwaka wa fedha kuanza.
Katibu Mkuu wa CCM na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, anaendelea na ziara ya mikoa miwili inayolenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025, kukagua na kuhamasisha uhai wa CCM kuanzia ngazi ya shina, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia majawabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news