MORONI-Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini humo,Saidi Yakubu tarehe 17,2024 wametembelea kiwanda cha maji cha Aden kinachomilikiwa na Mfanyabiashara mwenye asili ya Tanzania, Khalil Bakhressa.
Bw.Bakhressa aliueleza ujumbe huo kuwa hivi sasa wanazalisha maji hayo kwa wingi zaidi na wako mbioni kuanzisha kiwanda cha maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa kwa kushirikiana na kampuni za Tanzania.
Kiwanda cha Aden ni miongoni mwa viwanda vikubwa vya maji nchini Comoro.