MORONI-Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu, leo amewasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa nchi hiyo,Azali Assoumani ambapo wamepata pia fursa ya kufanya mazungumzo kuhusu uhusiano wa nchi hizo mbili.
Balozi Yakubu ambaye aliwasilisha hati hizo za utambulisho kwa lugha ya Kikomoro jambo lililomfurahisha Rais Azali alitumia pia fursa ya utambulisho kuwasilisha pia salamu za Rais Samia Suluhu Hassan za hamu yake ya kuona ushirikiano wa Tanzania na Comoro unaongezeka.
Kwa upande wake Rais Azali alimueleza Balozi Yakubu kuwa Comoro inathamini uhusiano wa kidugu na kihistoria baina yake na Comoro na kuwa daima watauenzi uhusiano huo na kumtaka atumie uwepo wake kuboresha ushirikiano wa kibiashara,kiuchumi,kijamii na kisiasa pia.
Awali kabla ya uwasilishaji wa hati za utambulisho Balozi Yakubu alikagua gwaride la heshima lililoandaliwa.