Bandari ya Uvuvi Kilwa kutoa ajira 30,000

LINDI-Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema mpaka sasa mradi wa ujenzi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa Masoko imeshatoa ajira kwa vijana wapatao 570 ambao wanafanyakazi hapo huku akiongeza kuwa utakapo kamilika utatoa ajira 30,000 katika nyanja mbalimbali.Waziri Ulega amesema hayo alipotembelea kukagua maendelea ya ujenzi wa mradi huo unaofanyika wilayani Kilwa mkoani Lindi leo Julai 30, 2024.
“Leo nimekuja kutembelea huu mradi nimewakuta vijana wanafurahia kazi wanayoifanya. Vijana wa taifa zima watapata fursa ya kufanya, tunataraji vijana wasiopungua elfu 30 kutoka maeneo mbalimbali watapata ajira hapa, Tunamshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi huu ambao ni wa kilelezo kwa taifa letu,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news