BASATA yamfungia Babu wa TikTok

DAR-Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema limejiridhisha kuwa, Seif Kassim Kisauji (Babu wa TikTok) ametenda kosa la kimaadili wakati akitekeleza kazi zake za sanaa.
Aidha,limefikia maamuzi ya kumfungia kutojishughulisha kufanya kazi za sanaa ndani na nje ya Tanzania kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julai 22,2024.

Vile vile, BASATA limemtoza faini ya shilingi milioni 3 ambayo anatakiwa kuilipa ndani ya siku saba kuanzia Julai 22,2024.

Kwa mujibu wa baraza hilo limefikia uamuzi huo baada ya kumuita Babu wa TikTok kuhusiana na ukiukwaji wa maadili akiwa kama nsanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa kwa usajili Na. BST-9684-2023-2154.

Imedaiwa ukiukwaji huo wa maadili ni kinyume na Kanuni ya 25 (6) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za mwaka 2018 na Mwongozo wa Uzingatiaji wa Maadili katika Kazi za Sanaa wa Mwaka 2023.

“Baraza la Sanaa la Taifa kupitia Sheria Na. 23 ya Mwaka 1984 na Maboresho yake ya Mwaka 2019 ina mamlaka ya kusimamia maadili ya msingi kwenye Sekta ya Sanaa kwa Kanuni ya 25(1)-(8) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018."

Pia, baraza limesema limekwishatoa na kuzindua mwongozo wa maadili katika kazi za sanaa ambao unapatikana katika tovuti yao.

Hivyo, ni jukumu la kila msanii na mdau wa sanaa na jamii kuzingatia maadili katika kazi za sanaa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news