Bonanza la Wizara ya Nishati lapamba moto Dodoma

DODOMA-Leo Julai 27,2024 watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake wameshiriki katika michezo mbalimbali katika Bonanza la Nishati Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Mgeni rasmi katika Bonanza hilo ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu , Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Judith Kapinga na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.
Baadhi ya Michezo inayofanyika kwenye Bonanza hilo ni Kupokezana vijiti wanaume, Kupokezana Vijiti Wanawake, Rede, Karata, Riadha, Kukimbia na yai, Kukimbia ndani ya gunia, Kukimbia na maji kwenye glasi, Kupenya ndani ya pipa, Mpira wa miguu, Mpira wa Pete, Bao na Karata.
Katika picha ni matukio mbalimbali wakati wa Bonanza hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news