DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania imeendesha semina kuhusu utambuzi wa alama za usalama katika noti pamoja na namna sahihi ya utunzaji wa noti na sarafu kwa kundi maalum la wasioona jijini Dodoma.
Katika semina hiyo, washiriki walielimishwa jinsi ya kutambua noti halali kwa kutumia alama maalum za usalama ambazo zinaweza kuguswa au kuhisiwa kwa mikono.
Pia, walipata mafunzo kuhusu njia bora za kutunza noti na sarafu ili kuhakikisha zinadumu kwa muda mrefu na kusaidia kupunguza gharama za kuchapisha noti mpya kufidia zilizoharibika.