CAG aipa tano Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA)

DAR-Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere ameipongeza Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Huduma ya Sheria PPAA, Bi. Agnes Sayi wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Bw. Kichere ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea banda la PPAA katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Huduma ya Sheria PPAA, Bi. Agnes Sayi akiongea kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando amemueleza CAG kuwa, Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023 imeboresha masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja kupunguzwa kwa muda wa kushughulikia malalamiko na rufaa zinazotokana na michakato ya Ununuzi wa Umma kutoka siku 45 hadi siku 40.
“Mabadiliko ya Sheria ya Ununuzi yamekuwa yakifanyika mara kwa mara kwa lengo la kupunguza muda, kuongeza uwazi na usawa katika shughuli za ununuzi wa umma, kuongeza ushindani,”amesema Bi. Sayi.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Kadhalika, Bi. Sayi ameongeza kuwa PPAA imefanikiwa kuanzisha Moduli ya kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia kieletroniki ambapo moduli hiyo ipo katika mfumo wa ununuzi wa umma kieletroniki (NeST) ambapo kupitia moduli hiyo wazabuni wataawasilisha malalamiko yao kieletroniki jambo ambalo litasaidia kuokoa muda na gharama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news