Chagueni anayekubalika na jamii-Mheshimiwa Ridhiwani

PWANI-Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze,Mhe. Ridhiwani Kikwete ameishauri jamii kushiriki katika kufanya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kwa kuangalia na kuweka mbele uzalendo wao na sio kuchaguana kwa kujuana.
Mhe. Ridhiwani ameyabainisha hayo kwenye mkutano na wananchi wa eneo la Mkange wilayani Chalinze mkoani Pwani ambapo amewasisitiza kushiriki katika hatua zote za uchaguzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura mpaka siku ya kupiga kura katika vituo vutajavyoandaliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
"Hata kama kuna mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi ambaye yeye mwenyewe mnamuona wala hataki mambo hayo,lakini jamii pale inamtaja vizuri,mfuateni na mmwambie kama Bwana wewe mwenzetu kila tukikaa kijiweni tunasema kama kuna mtu mzuri wa kutuongoza basi ni Bwana yule pale ambaye ni wewe utatuletea mambo mazuri eneo letu ,basi mfuateni na mwambie ili tukisaidie chama chetu.
"Lakini kutafuta wale marafiki zenu ambao mnauza nao mapori,kutafuta marafiki zenu mnaofanya nao ubadhirifu wa mali za umma ni kukiingiza chama cha watu kwenye mtihani mkubwa sana.

"Mimi ninaamini viongozi nyinyi ambao ni wanachama hamtafanya kosa hilo,tuleteeni watu ambao tukifika hapa watu wanaendelea na shughuli zao tukisubiri siku ya kupiga kura,tunapiga kura na maisha yanaendelea," alisema Mhe. Ridhiwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news