Chagueni viongozi wa maendeleo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa-Dkt.Biteko

GEITA-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuchagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwenye uchaguzi mwaka huu ambao watakuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo na kutatua changamoto zao kwa haraka.
Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara kijiji cha Lyambamgongo wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
“Muda utakapofika tuwe tayari kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ili tuweze kuchagua viongozi wazuri wenye sifa za kuchaguliwa ambao watasaidia kuleta maendeleo.

"Tunataka jimbo la Bukombe libadilike kwa kuwa na watu wenye maono au mawazo mazuri yatakayosaidia utatuzi wa changamoto zinazotukabili,”amefafanua na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news