ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imepokea ugeni kutoka taasisi ya Kimataifa ya International Bluecross inayofanya kazi na Asasi ya Bluecross Society of Tanzania.
Kwa pamoja wamejadili kuhusu kuboresha shughuli za uelimishaji na huduma za jamii katika eneo la ukanda wa mikoa ya Kaskazini na kuweka mikakati madhubuti ya kulitekeleza hilo.
Aidha, kwa kushirikiana na wageni hao, wametoa elimu kinga dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa wanafunzi 45 wa Shule ya Sekondari Felix Mrema iliyopo Daraja Mbili jijini Arusha.