ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu juu ya tatizo la dawa za kulevya kwa jamii inayoishi mpakani Namanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido mkoani Arusha.
Makundi yaliyofikiwa ni Askari wa Jeshi la Akiba, Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Namanga,viongozi wa Serikali na wadau wa maendeleo pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Msikiti wa Al-Nuru uliopo mpakani hapo.
Mwisho, makundi hayo yote muhimu yalihamasishwa kuendelea kushirikiana na Mamlaka katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya mpakani kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)