DCEA yamdaka Mtanzania akiunganisha ruti ya Bujumbura kwenda Dubai akiwa na dawa za kulevya

NA GODFREY NNKO

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inamshikilia Mtanzania Mbaba Rabini Issa mwenye pasipoti namba TAE442718.

Issa alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchior Ndadaye jijini Bujumbura, Burundi akiwa na kiasi cha kilogramu 3.8 za bangi iliyosindikwa (skanka).
Hayo yamesemwa leo Julai 17,2024 jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Aretas Lyimo wakati akizungumza na wanahabari kupitia hafla fupi ambayo imejumuisha tukio la kuwapa tuzo wadau mbalimbali.

“Dawa hizo zilikuwa zimefichwa kwa kushonewa ndani ya begi la nguo, mtuhumiwa huyo alikamatwa akijiandaa kusafiri kuelekea Dubai ”

Kamishna Jenerali Lyimo amesema,kufuatia mikataba ya kikanda na kimataifa iliyosainiwa na Tanzania katika udhibiti wa dawa za kulevya,mhalifu yeyote wa dawa za kulevya atakayefanya uhalifu katika nchi zilizoingia makubaliano na kukimbilia moja ya nchi hizo atakamatwa.”

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, Skanka ni jina la mtaani linaloitambulisha aina ya bangi yenye kiwango kikubwa cha sumu ya Tetrahydrocannabinol (THC).

Aidha, skanka ina sumu zaidi ya asilimia 45 ikilinganishwa na asilimia tau hadi 10 zilizopo katika bangi ya kawaida, hivyo skanka inatajwa kuwa na madhara makubwa zaidi kwa mtumiaji ikiwemo kuamsha matatizo ya afya ya akili.
Sehemu ya kemikali bashirifu iliyokamatwa na mamlaka hiyo.

Wakati huo huo, Kamishna Jenerali Lyimo amesema mamlaka hiyo kupitia ofisi zake za kanda zimefanyika operesheni katika mikoa ya Mwanza,Dodoma,Mtwara na Mbeya.

Operesheni hizo kwa nyakati tofauti amesema zimefanikisha kukamata gunia 285 za bangi kavu, kilo 350 za aina mbalimbali za dawa za kulevya.

Nyingine ni milimita 115 za dawa tiba zenye asili ya ya kulevya pamoja na lita 16,523 za kemikali bashirifu zilizokuwa zinasambazwa kinyume cha sheria.

Kamishna Jenerali Lyimo amesema, kupitia operesheni hiyo watu 48 wamekamatwa na mamlaka hiyo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news