SINGIDA-Naibu Waziri wa Madini,Dkt. Steven Kiruswa ameupongeza mkoa wa Singida kwa kuvuka lengo walilopangiwa kukusanya kwa asilimia 145.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Afisa Madini Mkazi mkoa wa Singida Mha. Sabai Nyansiri, Dkt. Kiruswa alisema kuwa awali mkoa wa Singida ulipewa lengo la makusanyo shilingi bilioni 12, lakini hadi kufunga mwaka wa fedha 2023/24 Ofisi hiyo ilikuwa imekusanya shilingi bilioni 18. Hii ni kutokana na juhudi zilizowekwa na huu ni mfano wa kuigwa.
Pia, Dkt.Kiruswa aliupongeza Mgodi huo kwa utekelezaji wa Mpango wa Wajibu wa Mgodi kwa Jamii inayozunguka mgodi kwa kufanikisha mradi wa ujenzi wa nyumba za jamii , madarasa ya shule na kuweka mifumo mizuri ya utunzaji mazingira katika eneo la mgodi.
Kwa upande wake , Mkuu wa wilaya ya Ikungi Thomas Apson aliishukuru wizara ya madini kupitia miradi ya kimkakati katika wilaya ya Ikungi na aliomba wizara kuendelea na utafiti wa madini ili kugundua maeneo mapya ya madini kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili wachimbe kwa uhakika bila kuleta migogoro .
Katika ziara hiyo Dkt.Kiruswa aliambatana na wataalam kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa.