Dkt.Mataragio akagua ujenzi wa kituo mama cha kujaza gesi

DAR-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amekagua kazi za ujenzi wa Kituo cha Kujazia Gesi kinachojengwa katika barabara ya Sam Nujoma mkoani Dar es Salaam na kumtaka Mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi kwa kuongeza rasilimali watu na vifaa.
Dkt. Mataragio amesema hayo tarehe 1 Julai 2024 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo. Amesema watanzania wanasubiri mradi husika kwa hamu kubwa hasa katika kipindi hiki ambacho agenda kuu ya Serikali ni matumizi ya nishati safi na salama.
Amesema,kituo hicho ndiyo kitakuwa Kituo Mama cha kujaza na Kusambaza gesi katika mikoa mbalimbali kwa kuanza na mikoa ya Dodoma na Morogoro pia kusambaza gesi katika vituo vingine vidogo vitakavyojengwa ikiwemo eneo la Muhimbili na Kibaha na baadaye katika maeneo mengine.

Ameeleza kuwa lengo la mradi huo ni kusogeza karibu huduma ya upatikanaji wa gesi kwa wananchi ili kuongeza kasi ya matumizi ya nishati hiyo.
Ili kuharakisha ujenzi wa mradi husika amemtaka Meneja wa Usimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini( TPDC), Mhandisi Aristides Katto kuwepo eneo hilo la mradi muda wote ili aweze kuona na kusimamia kazi hiyo kwa ufanisi na kutoa msukumo kwa mkandarasi kuharakisha ujenzi huo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango na Utekelezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Derick Moshi amesema kuwa mwezi Septemba mwaka huu kazi za awali za mradi huo zitakuwa zimekamilika, vifaa vitakuwa vimefika nchini na kuanza kusimikwa katika mradi huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news