Dkt.Mwasaga, Akili Mnemba tuiogope au tuikumbatie? Tuikumbatie

NA GODFREY NNKO

MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya TEHAMA nchini, Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema, hakuna sababu za kuiogopa Akili Mnemba (AI) badala yake tunapaswa kuikumbatia kwani ina matokeo chanya mengi.
Dkt.Mwasaga ameyasema hayo Julai 18, 2024 wakati akifanya mahojiano na Salim Kikeke kupitia Kipi cha Kasri la Kikeke ambacho huwa kinarushwa na Crown Redio iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Yafuatayo ni baadhi ya maswali kutoka kwa Salim Kikeke na majibu kutoka kwa Dkt.Nkundwe Mwasaga wakati wa mahojiano katika kipindi hicho;

1:Akili Mnemba tuiogope au tuikumbatie?

Dkt.Nkundwe

Akili Mnemba tunatakiwa tuikumbatie kwa sababu Dunia siku zote inaenda mbele. Teknolojia imekuja kama teknolojia nyingi ambazo zilishakuja tangu mwanzo.

Kinachotakiwa tujiandae tufanye ubunifu katika eneo hilo ili kufanya vitu vikubwa. Upande wetu Serikali tunaangalia teknolojia yoyote ambayo inafanya kazi na inaongeza pato kuu la Serikali.

2: Inatengeneza kazi au inaua kazi Mkurugenzi?

Dkt.Nkundwe...inatengeneza kazi.

3:Umesema Serikali inakumbatia suala hilo, tumeona mataifa yaliyoendelea ujio wa Akili Mnemba wanauchukua kwa tahadhari kubwa sana.Na wanataka kuwe na kanuni na udhibiti kwamba isizagae, hapa kwetu sisi tuna mikakati gani?.

Dkt.Nkundwe

Unajua ukiangalia katika eneo la Akili Mnemba linavyopokelewa na nchi mbalimbali duniani cha msingi ni kuangalia hizo nchi zina uwezo gani katika eneo hilo la kiteknolojia.

Zile nchi ambazo zina uwezo mkubwa wa kufanya ubunifu wao mara nyingi wana promote.
Zile ambazo zipo nyuma nyuma kidogo katika eneo hilo katika nchi zinazoendelea wenyewe wanapenda ku-regulate.

Wanaangalia sana mambo ya ethics, bias na vitu vingine ambavyo watu wanaona ni vya msingi hasa kulinda masoko yao na kulinda watu.

Sisi hapa ukiangalia tunachukua vyote viwili kwa pamoja kwamba tuna promote kwa vijana wafanye innovation kwa sababu hii ndiyo teknolojia ambayo ipo.

Na vile vile tunaangalia sasa masuala ya ulinzi wa taarifa binafsi, faragha za watu na mambo mengine ambayo yanaonekana yanaletwa na hii teknolojia.

Lakini ukiangalia kwa ujumla wake hii teknolojia ni teknolojia nzuri na ina fursa nyingi sana katika kuleta vitu vizuri katika uchumi zetu kama Tanzania.

Cha msingi ni kwamba, nchi ambayo itaipokea kwa haraka na inatengeneza mazingira ambayo Akili Mnemba inaweza kutumika vizuri ndiyo itakuwa ina future kubwa katika kanda au Kiafrika na sehemu zingine.

Na sisi tupo tayari kuhakikisha kwamba tunakuwa tunaongoza katika eneo hilo. Kwa mfano Mahakama ya Tanzania imeanza kutumia Akili Mnemba muda wala siyo kwamba ni mwaka huu.

Wenyewe wamekuwa wa kwanza kutokana na ufuatiliaji wetu inaonekana ni wa kwanza kwa Afrika.

4: Wasiwasi wangu ni kwamba tusije tukaziachia mashine zisije zikatutawala sisi, maana yake zikafanya kila kitu sawa.

Dkt.Nkundwe

Hilo,jambo ndiyo watu wengi wanatengeneza hofu kwa ujumla. Unajua Akili Mnemba ziko za aina tatu.

Kuna ile ambayo unaiandikia sheria inafanya kama inavyofanya. Kuna hii nyingine ambayo sasa hivi ambayo imepata sifa kubwa sana ambayo inaweza kutengeneza text, video.

Lakini, kuna ya tatu ile ambyo ninasema ina uwezo kama wa binadamu tunaita Super Intelligence huko hatujafika bado.

Kwa sababu Akili Mnemba haijawa na nafsi,binadamu ana nafsi.

5:Lakini...nafsi ipo njiani?...Yes, lakini kuna limitation ambazo zipo kwa mfano kuna limitation ya uwezo wa kuchakata.

Kuna limitation ya idadi ya data ambazo zipo na logarithms ambayo ndiyo ina drive hiyo Akili Mnemba.

Bado kuna limitation kwa sababu ya uwezo wa binadamu. Binadamu ana uwezo mkubwa kwa hiyo mpaka sasa hivi bado.

Hizo mashine tunazoziona kwa mfano roboti wengi wana uwezo wa mtoto wa miaka mitatu

Kwa hiyo anahitaji mtu wa kum-control , hauwezi kumchukua mtoto wa miaka mitatu ukamwambia aende mjini kutoka hapa (Mikocheni).

Kwa sababu ukitoka nje ya nyumba yako tu unaanza kukutana na sheria nyingi za kuvuka barabara, kuongea na watu na vitu vingine.

Maisha yetu yapo complex kidogo. Tunachukulia tu mfano unapotoka hapa tunakutana na sheria nyingi maana yake kuna sheria za haki za binadamu na roboti bado haijafikia huko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news