ZANZIBAR-Waziri wa Fedha, Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) amekuwa mgeni rasmi katika Mechi ya Hisani ya Ufunguzi wa mashindano ya '’PBZ YAMLE YAMLE CUP 2024'’ Msimu wa 6, Iliyowakutanisha Mazombi Fc dhidi ya Mboriborini Fc Katika uwanja wa Amaan Stadium, Visiwani Zanzibar, ambapo timu ya Mazombi FC imeibuka kidedea kwa kushinda kwa mikwaju ya penati 4 dhidi ya 2.
Akizungumza katika mchezo huo, Dkt.Nchemba amezipongeza timu zote mbili kwa kuonesha mchezo wa kiwango kikubwa na ameahidi Serikali itaongeza nguvu katika mashindano hayo.