Fahamu tofauti kati ya United Kingdom,England na Great Britain

NA DIRAMAKINI

SI mimi tu, pengine hata wewe huwa na maswali mengi na hata kujikuta unachanganya mafaili kuhusu United Kingdom,England na Great Britain.
Picha na Telegraph.

Mathalani yafaa kutambua kuwa England ni nchi kama ilivyo Tanzania huku mji mkuu wake mkuu ukiwa ni London, kama ilivyo Dodoma kwa Tanzania.

Kwa mantiki hiyo, Great Britain ni mjumuiko wa nchi tatu ambazo zimejumuika kwa pamoja kama nchi moja na mji wake mkuu ni London.

Nchi hizo ni;

1. England,

2. Scotland

3. Wales.

Aidha, unapoijumuisha Northern Ireland katika nchi hizo tatu ndipo inaundwa United Kingdom ikiwa ni Muungano wa nchi nne. Ikiwemo;

1. England,

2. Scotland,

3. Wales, na

4. Northern Ireland.

Kwa hiyo, mataifa hayo manne yakiwa katika Muungano huo mji wake mkuu ni London. Lakini, pale ambapo panahitaji uwakilishi wa kila nchi basi nchi hizo nne kila moja ina mji wake mkuu. Nchi na mji wake ni kama ifuatavyo;

1:Scotland mji mkuu ni Edinburgh,

2:Wales mji mkuu ni Cardiff;

3:Northern Ireland mji mkuu ni Belfast.

4:England mji mkuu ni London.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news