Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Julai 4,2024

DAR-Mhandisi Mkama Bwire ameteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaaam (DAWASA) katika kikao maalum cha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Bodi ya Wakurugenzi DAWASA kilichofanyika Juni 3, 2024 ofisi za DAWASA jijini Dar es Salaam.Mhandisi Bwire ni mtumishi wa Wizara ya Maji ambaye amehudumu kama Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Kibaha, Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) na hadi anapokea jukumu hili alikuwa ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini katika Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).
Uteuzi wa Bwire unakuja baada ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kumtaka aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA), Kiunga Kingu akae pembeni ya majukumu yake kwa muda, kuanzia Juni 30,2024 na akatangaza kuiweka DAWASA chini ya uangalizi maalum wa Wizara ya Maji ili kuboresha utendaji wake.














Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news