SONGWE-Mfamasia wa Kituo cha Afya cha Isansa kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Daudi Kwibuja (30) amefariki kifo cha kutatanisha na mwili wake kukutwa kando ya barabara kuu itokayo Mbeya kwenda Tunduma katika eneo la Mlowo wilayani humo.
Mwili wa mtumishi huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi katika Idara ya Afya umekutwa ukiwa na majereha mwilini mwake na tayari Jeshi la Polisi limeanzisha uchunguzi.
Akitoa taarifa ya kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Agostino Senga amesema kuwa, uchunguzi unaonesha mtumishi huyo aliuawa usiku wa Julai 3, 2024 na mwili wake kukutwa ukiwa umetupwa kando ya barabara hiyo Julai 4, 2024, majira ya asubuhi.
Kamanda Senga amesema, licha ya kuwa awali kudhaniwa kuwa marehemu alifariki kwa ajali ya kugongwa na gari, lakini baada ya mwili huo kuchunguzwa umekutwa na majeraha ambayo hayafanani na ya ajali ya kugongwa na gari.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo