DAR-"Shughuli ninazofanya mimi za Kamisaa wa Sensa zipo chini ya NBS, NBS ambayo ipo chini ya Wizara ya Fedha, kwa hiyo nimefanikiwa kutembelea mabanda ya Hazina yenyewe, sehemu ya mambo ya fedha, sehemu ya kulipa madeni, nimepita na taasisi zenu za mambo ya uhasibu.
"Nimependa sehemu kubwa hasa ile ya kulipa madeni, ku-control au kutoa elimu kuhusu deni la Taifa ambayo tunafikiria ni muhimu sana elimu hiyo iendelee kutolewa kwa sababu sisi wanasiasa mara nyingi tunayo tabia ya kugeuza maneno, kumbe hatujui kwamba masuala ya deni la Kitaifa yana utaratibu wake, na Tanzania hatujapita ile haki kwamba tumepita madeni, tupo kwenye level ya kawaida, kwa hiyo elimu iendelee kutolewa mara nyingi kusudi watu waweze kuelimika sahihi,"Kamisaa wa Sensa na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Semamba Makinda katika mahojiano na Hazina TV.