DAR-"Nimetembelea banda la Wizara ya Fedha, Wizara ya Fedha yenyewe pamoja na taasisi zake nyingi zipo ndani ya banda hili, kwa wananchi niwaambie maonesho ni mazuri sana, yana mambo mengi muhimu ukitaka elimu, ikiwemo elimu ya kodi, elimu ya fedha na kwa namna gani Serikali inafanya kazi, karibu Sabasaba.
"Katika banda la Wizara ya Fedha nimefurahi kutembelea kitengo cha kodi, moja mnatoa elimu ya kodi na tunajua kodi ni muhimu sana katika uchumi wa nchi yetu.
"Katika elimu ya kodi nimetembelea na nimejifunza ni kwa namna gani misamaha ya kodi huwa inatolewa.
"Miongoni mwa wanufaika wakubwa wa misamaha ya kodi ni wadau wote wa michezo ambao kupitia sheria iliyotungwa ya mwaka huu, tumepata msamaha wa baadhi ya vifaa vya michezo na kwa kuanzia mtambo wa VAR ambao umefungwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa,...tayari umeshafungwa na tayari watu wameshapewa mafunzo, Serikali imesamehe kodi ya mtambo ule ili wapenda michezo waweze kunufaika,"amesisitiza Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt.Damas Ndumbaro katika mahojiano na Hazina TV.