HAZINA TV:Wizara ya Fedha ni kiungo muhimu katika uchumi wa Tanzania

DAR-Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga amesema, Wizara ya Fedha ni kiungo muhimu katika uchumi wa Tanzania.

"Kwanza,neno lenyewe tu Fedha. Fedha ndiyo chanzo cha ukuaji wa uchumi, hakuna miradi inayoweza kufanyika au biashara bila Fedha, kwa hiyo Wizara ya Fedha ni muhimu sana katika uchumi wowote. Lakini, pia Wizara ya Fedha ndiyo inayosimamia Benki Kuu, ndiyo pia inasimamia taasisi mbalimbali;
Ameyasema hayo kupitia Hazina TV katika mahojiano ambayo yameendeshwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Benny Mwaipaja alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha.

Ni katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news