DAR-Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Prof Ibrahim Hamis Juma tarehe 5 Julai,2024 ametembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lililoko kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Akiwa bandani hapo, Mhe. Jaji Mkuu alisifu jitihada za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu za kuamua kutafsiri sheria mbalimbali na kuwa lugha ya Kiswahili huku akitaka ufafanuzi kama baada ya tafsiri sheria zitakuwa zinapatikana kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
"Niwapongeze kwa kutafsiri sheria kutoka Kiingereza kuwa Kiswahili, zitakuwa zinapatikana kwa lugha ya kiswahili na kingereza?."
Akitoa maelezo kwa Mhe Jaji Mkuu wa Tanzania, Wakili Mwandamizi wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bi. Angella Kimaro amesema sheria hizo zitapatikana kwa lugha ya Kiswahili na kingereza.
"Sheria hizi Mhe. Jaji zitapatikana kwa lugha zote mbili kupitia mifumo yetu, pia katika wananchi watapa kuziona sheria zilizofanyiwa marekebisho kupitia madirisha yaliyoko kwenye mifumo yetu,"asema Bi.Angella.