SCOLA MALINGA
NA PETER HAULE
TANZANIA imepokea msaada wa nyongeza wa Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma baada ya marekebisho ya mikataba miwili ya msaada kati ya Tanzania, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Ubalozi wa Japan.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto) na Ujumbe wa Japan ukiongozwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa (kulia), ukiwa katika hafla ya kusaini mkataba wa nyongeza ya Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 kwa ajili mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigomailiyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Mikataba ya marekebisho ya msaada imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan Tanzania, Bw. Hitoshi Ara, kwa niaba ya Japan.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa, wakibadilishana mkataba wa Marekebisho ya msaada wa nyongeza ya Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 na kufanya jumla ya msaada kuwa shilingi bilioni 53.35 baada ya awali kutolewa shilingi bilioni 44.42 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma, hafla iliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kusainiwa kwa marekebisho ya mikataba hiyo, Dkt. Mwamba alisema kuwa, awali Serikali ya Japan kupitia mikataba iliyosainiwa Februari 4, 2022 ilitoa msaada wa Yen za Japan bilioni 2.73 sawa na shilingi bilioni 44.42 kwa ajili ya ukarabati wa Bandari hiyo.
“Jumla ya msaada uliotolewa na Serikali ya Japan unakuwa Yen za Japan bilioni 3.27 sawa na shilingi bilioni 53.35, ambapo fedha zilizoongezwa zinalenga kuziba pengo lililotokana na kuporomoka kwa thamani ya Yen za Japan na shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani,"ameeleza Dkt. Mwamba.
Alisema kuwa Mradi huo, utaboresha usalama na ufanisi wa shughuli za upakiaji wa abiria na upakuaji wa mizigo kwa kukarabati jengo la abiria la Bandari ya Kigoma na ujenzi wa ghala la kuhifadhia mizigo litakalo gharamiwa na Serikali ya Tanzania na kujenga barabara unganishi za kuingia na kutoka bandarini ambako kutachangia kuimarika kwa biashara na usafirishaji katika maeneo husika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Tanzania, Bw. Hitoshi Ara, wakionesha mkataba wa Marekebisho ya msaada wa nyongeza ya Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 na kufanya jumla ya msaada kuwa shilingi bilioni 53.35 baada ya awali kutolewa shilingi bilioni 44.42 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma, hafla iliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa, wakisaini mkataba wa Marekebisho ya msaada wa nyongeza ya Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 na kufanya jumla ya msaada kuwa shilingi bilioni 53.35, baada ya awali kutolewa shilingi bilioni 44.42 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma, hafla iliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akiihakikishia Japan kuwa Serikali itachukua hatua zote muhimu kuhakikisha mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma unatekelezwa kwa ufanisi baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Marekebisho ya msaada wa nyongeza ya Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Vilevile Dkt. Mwamba alisema kuwa upatikanaji wa fedha hizo ni mwendelezo wa ufadhili kutoka Serikali ya Japan katika miradi ya maendeleo ambapo Tanzania inanufaika katika maeneo ya sekta za Kilimo, Maji, Afya, Nishati, Usafirishaji, uendelezaji wa miji, elimu na Usimamizi wa Fedha za Umma.
Aidha, Dkt. Mwamba ameihakikishia Serikali ya Japan utayari wa Tanzania chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuendelea kuimarisha ushirikiano kwa maendeleo ya wananchi wa pande zote na kwamba itachukua hatua zote muhimu kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa, alisema kuwa wametoa msaada wa fedha za mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma kwa kuwa utasaidia katika ukuaji wa uchumi na masuala ya kijamii.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa, akieleza sababu za kutoa nyongeza ya Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 kwa ajili mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma kuwa ni pamoja na mabadiliko ya viwango vya ubadilishaji fedha, baada ya kusainiwa kwa msaada huo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa, wakizungumza masuala mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Marekebisho ya msaada wa nyongeza ya Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Alisema kutokana na kushuka kwa kasi kwa viwango vya ubadilishaji wa fedha kwa miaka ya hivi karibuni na kupanda kwa gharama za bidhaa na mafuta kutokana na mgogoro wa Ukraine na Urusi, Serikali yake ilitambua kutakuwa na ukosefu wa fedha katika mipango iliyokuwa imewekwa awali ndio sababu ya kuongeza fedha za mradi huo.
Alisema kuwa Bandari hiyo ni kitovu cha usafirishaji katika nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia ikichochewa na miundombinu ya barabara na reli.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto), Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Tanzania, Bw. Hitoshi Ara (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Marekebisho ya msaada wa nyongeza ya Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto), Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Tanzania, Bw. Hitoshi Ara (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Ubalozi wa Japan baada ya kusainiwa mkataba wa Marekebisho ya msaada wa nyongeza ya Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto), Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Tanzania, Bw. Hitoshi Ara (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Ubalozi wa Japan baada ya kusainiwa mkataba wa Marekebisho ya msaada wa nyongeza ya Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha).
Mhe. Balozi Misawa, alisema nchi yake inashirikiana na nchi mbalimbali katika utekelezaji wa miradi ili kukuza Uchumi kupitia miundombinu madhubuti na kuongeza ushirikiano na anaamini kupitia marekebisho ya mikata hiyo, mradi utatekelezwa kwa ufanisi.