DAR-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, amesisitiza utoaji wa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria kwa wananchi.
Mhe. Jaji amesema hayo Julai 5,2024 alipotembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lililoko kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
"Endeleeni kutoka elimu kwa wananachi, hakikisheni wananchi wengi wanapata uelewa wa masuala haya kisheria, mshirikiane na Wizara ya Katiba na Sheria katika kutoa huduma ya msaada wa kisheria kupitia kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama samia ili muweze kuwafikia watu wengi zaidi," amesema Mhe. Feleshi.
Akipokea maelekezo ya Mhe. Feleshi, Wakili Mwandamizi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Angella Kimaro ameeleza mwenendo wa ushiriki wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika maoenesho hayo, ambapo amesema wananchi wamekuwa wakija kupata ushauri na wengi wao wakiwa wanataka kufahamu majukumu ya hiyo.
Tags
Habari
Maonesho ya 48 ya Biashara ya Sabasaba
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali