DAR-Viongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) wameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake kwa kuendelea kuelimisha na kuhabarisha wananchi na wadau juu ya masuala mbalimbali yanayotekelezwa na ofisi hiyo ikiwemo masuala ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Ajira na Ukuzaji Ujuzi.
Pamoja na Menejimenti ya Maafa, Uratibu wa shughuli za Serikali na fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 13, 2024 wakati walipotembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zake katika maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es salaam.
Aidha, viongozi hao wametembezwa na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na ofisi hiyo.
Tags
Habari
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT)
Maonesho ya 48 ya Biashara ya Sabasaba
Ofisi ya Waziri Mkuu