Serikali yalifunga Kanisa la Nabii Kiboko ya Wachawi

DAR-Serikali imeagiza kufungwa Kanisa la Christian Life Church linaloongozwa na Nabii Domique Kashoix Dibwe maarufu Kiboko ya Wachawi, lililopo Buza kwa Lulenge katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa ni baada ya kanisa hilo kwenda kinyume cha taratibu za usajili hapa nchini.

Barua ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia ya Julai 25, 2024 imewaelekeza Mwenyekiti wa Kanisa la Christian Life Church na Mchungaji Dominique Kashoix Dibwe kufunga tawi la kanisa hilo linaloendeshwa na mchungaji huyo.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa za kufungwa kwake ni kutoa mafundisho yenye kuleta taharuki katika jamii na mahubiri ambayo ni kinyume na maadili, mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania.

Madai mengine ni kutoa mahubiri yanayodhalilisha watu madhabahuni, kutoa mahubiri chonganishi na kuhamasisha waumini wa kanisa lake kuua watu kwa dhana au tuhuma za uchawi au ushirikina.

Baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Serikali imeagiza kufungwa Kanisa hilo, baadhi ya vitu kanisani hapo vimeondolewa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news